Numbers 12:6-8

6 a Bwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,
nitajifunua kwake kwa maono,
nitanena naye katika ndoto.

7 bLakini sivyo kwa mtumishi wangu Musa;
yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

8 cKwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo la Bwana.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Musa?”

Copyright information for SwhKC